Upanuzi wa Ufalme Mfululizo
Vifaa rahisi, tendaji na vya nguvu vya
kupanua Ufalme wa Mungu.
· Injili Kulingana na Yesu Kristo
· Kuwafanya Wanafunzi Wafanyao Wanafunzi
· Kupanda Ushirika wa Nyumbani
· Kuwafikia ambao hawajafikiwa
· Kuwahudumia Waislamu
Katika Misururu ya Upanuzi wa
Ufalme, utaona maelezo na hadithi za kusisimua, na
mifano ya kawaida, ambayo imeundwa kukusaidia ujifundishe, ufuate, na kupokeza kwa vizazi vijavyo vya wanafunzi.
Hizi nyenzo ziliandikwa kusudi ziwe zenye maana na vipengee muhimu pekee. Hizi nyenzo hazina uzito wa
kukuchanganyisha. Mafunzo yametengenezwa rahisi ya kujifundisha, kutumia, na kufundisha kizazi
kijacho.
Katika kitabu cha kwanza, Injili Kulingana na Yesu Kristo, utawakilishwa na Injili nyororo iliyofundishwa
na Yesu na mitume na ikaishi na kanisa la kwanza. Kuwa wa kwanza kujifunza imani ambayo ilibadili kwa ukubwa mno
vizazi vya wafuasi wa Kristo, wanaume na wanawake walioupindua ulimwengu juu chini.
Katika kitabu cha pili, Funguo
za Upanuzi wa Ufalme, utakusanya habari na mshawasha jinsi wewe binafsi unaweza kuchangia kwa
utimilizaji wa Wito Mkuu katika kizazi hiki. Utatiwa changamoto na kuhamazishwa kusalimisha kila kitu kwa
Kristo, na kwenda kule inje kuwafanya wanafunzi. Vifaa vya kupitia orodha ya kiroho vimepeanwa kukuongoza wewe
kufikia upeo kamili wa uhuru toka dhambini. Ndio, utaona kwamba uhuru toka dhambini ni ukweli wa kimatendo, na
sasa unaweza kuufikia.
Kitabu cha tatu, Kanisa Ndani
ya Nyumba, kitakuonyesha matendo ya Agano Jipya ya ushirika wa nyumbani. Utajifunza sehemu za
kibiblia, utendaji, na kiunabii za kukurejesha kwa urahisi wa matendo ya kanisa yaliyo hai.
Misururu ya Upanuzi wa Ufalme pia ina nyongeza mbili: ya kwanza itakufundisha jinsi ya kupanda ushirika katika maeneo ya
watu ambao hawachafikiwa vile Yesu alifanya, jinsi imewakilishwa katika Luka Sura ya 10. Ya pili itakuonyesha
jinsi ya kumwakilisha Kristo kwa Waislamu kwa urahisi ukitumia Korani.
Email us at info (at) kingdomdriven (dot) org to obtain copies of
this book in either Swahili or English in East Africa.
Hadithi Za Mchungaji
Kuwafundisha Wachungaji Wapya na Makutano Wapya
Rob Thiessen, Anne Thiessen na George
Patterson
Je, unataka nyenzo rahisi , tekelezi na ya Kibiblia ya kuanzisha msururu wa kanisa la kuzalisha?
Katika kitabu cha Hadithi za Mchungaji ndimo kuna nyenzo hiyo moja tu!
Njia
rahisi ya kuzalisha--kutumia Hadithi.
Mafundisho mwafaka kwa mtu binafsi au familia nzima.
Kinaweka msingi dhabiti wa Kibiblia.
Toleo
la Agano Jipya lililo hai
Kitabu cha
Hadithi za Mchungaji kinafundisha misingi ya uinjilisti,
huduma ya mafunzo na kuanzisha makanisa mapya kwa kutumia Hadithi za uerevu za Kibiblia.
Hadithi hizi zinashughulika karibu na kila hali ya kawaida ya kihuduma inayoweza fikirika, na bila kutumia jitihada
zozote, kinaonyesha jinsi tunavyoweza tekeleza mafundisho ya uteuwa ya Yesu.
Vitabu vingi vinavyo jaribu kufunza itikadi za kufaulu kwenye huduma vimeandikwa kama somo la darasani au kitabu
cha mwanafunzi. Lakini hivi si ndivyo Yesu alifundisha. Juu ya yale maagizo rahisi ya msingi aliyowapa wafuasi
wake, Yesu alitoa hadithi, tena nyingi sana! Hadhiti zake sinarudiwa hata leo, na bado zina badili maisha.
Kitabu hiki kinapendeza wasomi wa tabaka na umri mbali mbali na wa tamaduni zote.
Mwanzoni kiliandikiwa waumini wapya kwenye uwanja wa kiutume, lakini kinavutia sana na kinatumika kwa nchi kadhaa
tofauti tofauti kufunza itikadi sisizopitwa na wakati za huduma wa Agano Jipya.
This book is not currently in print in Swahili, but may be downloaded for free in
Swahili here.
If you would like to help sponsor getting this book in print in Swahil, consider
making a donation.
|